Public Notice
Posted On: Aug 07, 2019
Tahadhari ya uwepo wa matapeli kwa wateja wa TMDA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA

TAARIFA KWA UMMA

31 Julai, 2019

TAHADHARI YA UWEPO WA MATAPELI KWA WATEJA WA TMDA

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwatahadharisha wateja wake kuwa wamejitokeza watu ambao hujifanya kuwa ni watumishi wa TMDA na kuonesha nia ya kuwasaidia wateja wanaohitaji huduma kwa lengo la kuwatapeli.
  2. Watu hao ambao ni matapeli wamekuwa wakiwasumbua wateja kwa njia ya simu za mkononi wakiwataka kuonana nao nje ya Ofisi na katika muda ambao siyo wa kazi au kuwataka watume pesa kwa njia ya simu ili huduma walizoomba zifanyiwe kazi kwa haraka.
  3. TMDA kupitia ofisi ya Makao Makuu na Ofisi zake za Kanda, inapenda kuutarifu umma kuwa huduma zote zitolewazo na TMDA hazitolewi kwa kificho au nje ya Ofisi za TMDA, hivyo inapotokea mtu anakushawishi akupe huduma kwa utaratibu tofauti na ulioainishwa hapo juu, tafadhali toa taarifa mara moja katika Ofisi zetu za Makao Makuu na Kanda. Hivyo watu wenye kuonesha dalili za kutaka kutoa msaada kwa kujificha au nje ya Ofisi za TMDA sio watumishi wa Mamlaka.
  4. Ikumbukwe kuwa huduma za TMDA hutolewa na watumishi wenye vitambulisho halali na waliopo katika ofisi zetu tajwa hapo juu au Kituo cha forodha na kwamba malipo yote ya ada na tozo kwa huduma zitolewazo hufanyika kupitia benki au mawakala waliothibitishwa wa benki husika baada ya kupatiwa ankara kifani (Profoma invoice) na Namba ya Malipo ya Serikali (Control Number).
  5. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia ofisi za TMDA Makao Makuu au Ofisi za Kanda zilizopo Dar Es Salaam, Mwanza, Simiyu, Arusha, Mbeya, Dodoma, Mtwara na Tabora au kupiga simu bila malipo kupitia Na. 0800110084.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),
Mtaa wa Mwanza, Kitalu T, Kiwanja Na.6
S.L.P 1253, Dodoma Au
S.L.P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Simu bila Malipo: 0800110084